0

Simba yajitetea kwa FCC

C560a197d01493147f919e1a0667ca23.jpeg Simba yajitetea kwa FCC

Sat, 21 Nov 2020 Source: HabariLeo

KLABU ya Simba imejitetea kwa Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC) baada ya kudaiwa kuchelewesha kukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo.

Taaarifa hiyo imetolewa na Klabu ya Simba kujibu barua ya FCC iliyotolewa juzi ikidai kuwa mchakato mzima wa mabadiliko ya klabu hiyo umekuwa ukikwamishwa na Simba, ambao wameshindwa kutekeleza maagizo.

“Tunaandika kueleza kusikitishwa kwetu na taarifa ya Tume ya Ushindani wa Biashara ya tarehe 8 Novemba, 2020 iliyotolewa kwa umma ikidai kwamba sababu ya kuchelewa kukamilika kwa mchakato mabadiliko zinatokana na Klabu ya Simba wenyewe, “ imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya Simba iliyotolewa jana.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa Klabu ya Simba imekuwa na mawasiliano chanya na FCC kupitia vikao mbalimbali na wamekuwa wakiendelea kuwasiliana hadi hivi karibuni.

Klabu hiyo imefafanua zaidi kuwa taaarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji Novemba 15, 2020 kwa waandishi wa habari juu ya mchakato wa manabadiliko ulipofikia kwa sasa mchakato huo upo FCC na si kwamba FCC wanakwamisha au kuchelewesha mchakato huo.

Simba imesema kuwa inaheshimu sheria za nchi na wakati wote itafuata matakwa ya kisheria katika uendeshaji wa masuala ya Klabu. Klabu pia inatambua na kuheshimu mamlaka ya FCC na Mkurugenzi wa FCC katika kukamiisha mchakato huo.

Klabu hiyo imesema kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa FCC na taasisi zingine za umma, ambapo wameombwa na kuwasilisha taarifa nyingi kuhusu suala hilo na wako tayari kuendelea kutoa taarifa zilizo ndani ya mamlaka ya uwezo wao (Simba) ili kukamilisha zoezi hili.

Chanzo: HabariLeo