0

Simba waanza mazoezi, kujipima Jumatatu

Simba waanza mazoezi, kujipima Jumatatu

Thu, 12 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Thobias SebastianKikosi cha Simba jana Jumatano Novemba 12 kilianza mazoezi kwa wachezaji waliokuwepo baada ya mapumziko ya siku tatu mara baada ya kucheza mechi na Yanga.

Kikosi hiko cha Simba kitacheza mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya African Sports kutokea Tanga inayoshiriki Ligi Daraja La Kwanza.

Mechi hiyo ya kirafiki itachezwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi  itakayoanza saa 11:00 jioni na kiingilio kitakuwa Sh 3,000 mzunguko na Sh 5,000 VIP.

Ukiachana na wale wachezaji waliokwenda katika majukumu ya timu zao za taifa na waliokuwa majeruhi wengine waliobaki watakuwepo.

Miongoni wa wachezaji ambao watakuwepo ni Benno Kakolanya, Ally Salim, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Pascal Wawa, Kennedy Juma, Larry Bwalya na Ibrahim Ajibu.

Wengine Bernard Morrison, Miraji Athumani, Francis Kahata, Hassan Dilunga na Charles Ilanfya.

Chanzo: Mwanaspoti