0

Simba vs Namungo, Shoo ya Kiufundi, Simba imeiva

Simba vs Namungo, Shoo ya Kiufundi, Simba imeiva

Tue, 1 Sep 2020 Source: Mwanaspoti

By Charles AbelREKODI mpya mbili zimeandikwa na Simba ambazo ni kuwa timu iliyotwaa mara nyingi taji la Ngao ya Jamii, lakini nyingine ni ile ya kuwa timu iliyotwaa taji hilo mara nyingi mfululizo ambapo imelichukua mara nne.

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa jijini Arusha juzi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, uliwawezesha kutwaa taji hilo kwa mara nyingine baada ya kulichukua katika miaka ya 2019, 2018, 2017, 2012 na 2011.

Kiwango bora cha nyota mpya wa Simba, Bernard Morrison, kilitosha kuamua matokeo ya ushindi kwa timu yake akihusika katika mabao yote mawili yaliyofungwa katika mchezo huo ambapo, moja lilifungwa kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na John Bocco ambayo ilitokana na Morrison kufanyiwa faulo ndani ya eneo la hatari la Namungo.

Na bao la pili la Simba lilifungwa na Morrison mwenyewe katika dakika ya 60 ya kipindi cha pili cha mchezo huo akiunganisha vyema kwa mguu wake wa kulia, pasi ya Clatous Chama.

Mwanaspoti ilitazama mchezo na hapa inajaribu kuainisha masuala kadhaa yaliyojitokeza kuanzia dakika ya kwanza hadi filimbi ya kumaliza mchezo ilipopulizwa na mwamuzi, Ramadhan Kayoko kutoka Dar es Salaam.

TIMU BORA ZAIDI

Chanzo: Mwanaspoti