0

Simba, Yanga mziki ndio huu!

Simba, Yanga mziki ndio huu!

Fri, 6 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By CHARLES ABEL MBINU za kiufundi zina nafasi kubwa katika kuamua matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kwa namna zinavyofanyiwa kazi na wachezaji ndani ya uwanja.

Iwapo wachezaji watazifanyia kazi vyema na kwa ufanisi mkubwa mbinu, timu inakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi lakini kinyume chake, uwezekano wa kupoteza mechi huwa ni jambo linalotegemewa.

Kesho Jumamosi, timu za Yanga na Simba zitaumana katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na ambao siku zote umekuwa na msisimko mkubwa na hapana shaka yapo sasa mabenchi ya ufundi kwa kila timu yanaumizwa kichwa kujua vikosi vyao viingiaje katika mechi hiyo ili wapate ushindi.

Ingawa mara nyingi mipango na mbinu hubadilika kwa kila timu pindi Simba na Yanga zinapokutana, mechi zilizopita za Ligi Kuu msimu huu baina ya timu hizo, zinatoa uwezekano wa mambo kadhaa kufanywa na benchi la ufundi kwa kila katika mchezo huo.

Vikosi

Yanga inaelekea katika mchezo huo ikiwa na bahati nzuri ya kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ambao wako fiti na tayari kwa mchezo huo wa watani wa jadi kulinganisha na Simba jambo ambalo linaweza kuwa na faida kwao kwa kiasi fulani.

Chanzo: Mwanaspoti