0

Simba, Yanga fulu sapraizi

Fri, 6 Nov 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

MECHI za watani wa Jadi, Simba na Yanga huwa zina mambo mengi lakini hakuna kitu kinachosuuza mioyo ya mashabiki, viongozi na wachezaji wa klabu hizo zaidi ya kupata ushindi kila zinapokutana.

Hata hivyo, katika mechi baina ya timu hizo kuna mambo huwa yanatokea ambayo yanaacha alama ambazo zimeendelea kudumu kwa vizazi na vizazi.

MPIRA KWAPANI

Simba ndio timu iliyoacha alama ya kuingia mitini mara nyingi katika mechi za watani wa jadi kwani, mara mbili imeweka mpira kwapani dhidi ya Yanga. Machi 3, 1969, Yanga ilipewa ushindi wa chee wa mabao 2-0 baada ya Simba wakati huo ikijulikana kama Sunderland kugoma kuingia uwanjani.

Pia, Novemba 13 mwaka 1991 Yanga ilipewa ushindi wa bure wa mabao 2-0 baada ya Simba kugoma kurejea uwanjani katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.\Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Simba ilikuwa imeshachapwa bao 1-0 lakini cha kushangaza timu zilzipokwenda mapumziko, Wekundu wa Msimbazi hawakurejea uwanjani kuendelea bila kutoa sababu.

HAT TRICK PEKEE

Chanzo: mwanaspoti.co.tz