0

Shinyanga, Lindi zang’ara Umitashumta

7373717f76f7bf72d639baed2b1d11c8.jpeg Shinyanga, Lindi zang’ara Umitashumta

Thu, 10 Jun 2021 Source: www.habarileo.co.tz

TIMU za soka za Shinyanga, Lindi na Songwe zimeanza vizuri mashindano ya 25 ya Umoja wa Michezo na Taaluma ya Shule za Msingi (Umitashumta) yanayoendelea mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa matokeo ya siku mbili yaliyotumwa na Msemaji wa mashindano hayo John Mapepele, Shinyanga kawaida ilishinda michezo miwili ya ufunguzi dhidi ya Mwanza bao 1-0 na wa pili wa jana dhidi ya Mara mabao 4-0.

Aidha, Shinyanga maalum pia, ilifanya vizuri kwenye soka baada ya kushinda mabao 5-0 dhidi ya Kagera. Timu nyingine zilizofanya vizuri kwenye mchezo huo ni Mbeya iliyoifunga Morogoro mabao 3-1, na Mtwara mabao 2-0 dhidi ya Njombe.

Nyingine ni Simiyu 4-0 dhidi ya Arusha, Songwe ikishinda michezo miwili dhidi ya Kilimanjaro mabao 4-2 na dhidi ya Arusha 7-4, Kigoma ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Lindi mchezo wa awali na Mwanza na Kilimanjaro zikitoka sare ya bao 1-1.

Kwa upande wa wasichana katika soka, Lindi iliifunga Kilimanjaro na Katavi kila mmoja mabao 2-0, Geita iliifunga Kilimanjaro 2-0, Mwanza 4-2 Singida, na 1-0 dhidi ya Rukwa.

Katika mchezo wa netiboli, Mara ilishinda mabao 34-14 dhidi ya Iringa, Geita 24 na Morogoro 10, Kigoma 22-20 dhidi ya Mtwara, Lindi 15-06 dhidi ya Kilimanjaro, Rukwa 14-08 dhidi ya Ruvuma na Katavi 07-06 dhidi ya Manyara.

Michezo ya ufunguzi, Lindi ilishinda 14-08 dhidi ya Iringa, Tabora 27-10 dhidi ya Njombe, Tanga 3417 dhidi ya Dar es Salaam na Simiyu 18-13 dhidi ya Arusha.

Mpira wa mikono timu zilizofanya vizuri ni Pwani, Njombe wasichana, Rukwa, Singida wasichana, Shinyanga wasichana, Tanga, Songwe , Mtwara huku Dar es Salaam ikifanya vibaya.

Kwa upande wa wavu, Katavi, Dodoma, Shinyanga, Kagera, Kigoma, Mbeya wasichana na Dar es Salaam wasichana zimeanza vizuri na mchezo wa goli, Katavi, Tanga, Morogoro na Arusha pia, walianza vyema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz