0

Serikali- Mashabiki sasa kukata tiketi za msimu mzima

Serikali- Mashabiki sasa kukata tiketi za msimu mzima

Wed, 4 Nov 2020 Source: HabariLeo

MKURUGENZI wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na MIchezo, Yusuf Singo amesema Serikali ina mpango wa kuanzisha mfumo wa kuuza tiketi za msimu mzima kwa mashabiki wa soko nchini kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.

Mfumo huo wa tiketi za kieletroniki ulizinduliwa rasmi Septemba mwaka 2016 na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa wakati huo, Nape Nauye

Amesema kuwa mfumo huo una lengo la kuongeza mapato katika Uwanja wa Taifa kwa kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki ambapo wateja watahitajika kuwa na kadi za e-wallet pamoja na kufanya malipo kwa njia ya mtandao ili kuingia uwanjani.

Mfumo huo wa kielektroniki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa utawawezesha watu wote kuingia uwanjani ndani kwa wakati hivyo kuokoa muda wakati wa kuingia uwanjani.

Chanzo: HabariLeo