0

Rostam Azizi "sina mpango wa kununua hisa Yanga"

Thu, 10 Sep 2020 Source: millardayo.com

Mfanyabiashara maarufu na mwanachama wa klabu ya Yanga, Rostam Aziz amesema tetesi za kutaka kununua hisa katika klabu ya Yanga ni za kupuuzwa.

‘Nimeshangazwa na taarifa zinazoendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zinazodai niko tayari kuwekeza fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 13 na hivyo kununua asilimia 29 ya hisa katika klabu ya Yanga ambayo mimi ni mwanachama wake” Rostam

“Napenda kutumia fursa hii kutahadharisha umma na wana Yanga wenzangu kwamba, taarifa hizo hazina ukweli wowote. Taarifa kwamba nimetangaza uamuzi huo katika kikao nilichofanya na viongozi wa Yanga ni za uongo” Rostam

“Msimamo wangu kuhusu uendeshaji wa klabu yetu uko bayana kwamba, mimi si muumini wa Yanga kuuza hisa. Wana Yanga tunapaswa kuwa makini na usambazaji wa taarifa za namna hiyo katika mitandao ambayo imekuwa inatumika kuzusha kila aina ya habari.’ – Rostam

‘KIPUA’ STAA ANAEHESHIMIKA KWAO, AMEFANYA TAMASHA IKULU, MREMBO ANAEMMILIKI, ANAJAZA UMATI

Chanzo: millardayo.com