0

Ramadhani Singano, ilivyokuwa Mazembe mpaka Nkana Fc

Ramadhani Singano, ilivyokuwa Mazembe mpaka Nkana Fc

Thu, 5 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIPA ASSA MAZINGIRA yana nafasi kubwa ya kutengeneza ndoto za mtu baadaye, ukitaka kuamini hilo, muulize Mtanzania Ramadhan Singano ‘Messi’ anayecheza Nkana FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia (MTN).

Hakukurupuka kuingia kufanya kazi ya soka, ni kitu ambacho kilikuwepo kwenye familia yake. Mwanaspoti limefanya mahojiano maalumu na Messi, ambaye amesimulia namna alivyokuwa akiwaona kaka zake wakicheza soka na hapo akapata mzuka na kuwafuata kila wanapokwenda kucheza mechi.

“Mazingira ya familia ndio sababu ya kucheza soka ndio maana inaweza kuwa ngumu ukiniuliza isingekuwa soka ningefanya kazi gani, nilikuwa natoroka shule ili mradi tu nikacheze,” anasema ambaye amewahi kuzichezea Simba na Azam.

MAISHA YA TP MAZEMBE

Anafichua faida za kutoka nje ya mipaka ya Tanzania jinsi kunavyotafsiri kiwango chake, kujua thamani yake, kujifunza ni vitu gani anatakiwa kuvifanya ili kufaidi matunda ya kipaji.

“Japokuwa TP Mazembe sikupata nafasi ya kucheza kutokana na ushindani wa namba kwa wachezaji niliowakuta, pamoja na hilo akili yangu imefunguka kutambua mimi ni nani. Hilo limetokana na aina ya maisha niliyoyakuta kwa wachezaji wa DR Congo, mitazamo yao ya kazi na maisha kwa ujumla,” anasema Singano na anaongeza kuwa,

Chanzo: Mwanaspoti