0

Ndondo hatua ya 16 kuanza kesho

Wed, 9 Sep 2020 Source: habarileo.co.tz

MASHINDANO ya ndondo yanaoneshwa katika kisimbuzi cha DSTV chaneli namba 294, yanatarajiwa kuingia hatua ya 16 kuanzia Septemba 10.

Mratibu wa mashindano hayo, Daudi Kanuti alisema mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Keko Mwanga na Lumo utakaochezwa Uwanja wa Bandari, Temeke. Timu zilizofuzu 16 kutoka Kundi A ni Black Six na Twiga International, Kundi B ni Banda FC na Kinondoni Utd, Kundi C ni Uruguay FC na Mamu Pharmacy, Kundi D ni Sifa FC na Kimara Kombaini.

Kutoka Kundi E ni Lumo Kombaini na IBDHU FC, Kundi F ni Mbeya Boys na Keko Mwanga, Kundi G ni Mabibo Market na Magomeni Kombaini na Kundi H ni Toroli Kombaini na Zofa FC.

Kwa upande wa wafungaji wanaoongoza ni Moses Kitandu wa Black Six mwenye mabao sita, Mashaka Pogba wa Kinondoni Utd mwenye mabao matano.

Wenye mabao matatu ni Tidy Gideon na Ramadhani Mchinga wote wa Lumo Kombaini, Hamim Musa wa IBDHU na Ton Mwangila wa Mbeya Boys.

Chanzo: habarileo.co.tz