0

Naomi ashinda taji la Grand Slam

Naomi ashinda taji la Grand Slam

Mon, 14 Sep 2020 Source: HabariLeo

MCHEZAJI wa tenisi, Naomi Osaka ameonesha kukomaa baada ya kumfunga Victoria Azarenka katika mchezo wa fainali wa US Open na kushinda taji la tatu la Grand Slam.

Naomi raia wa Japan mwenye umri wa miaka 22, alishinda 1-6 6-3 6-3 likiwa taji lake la pili la US Open. Naomi alizidiwa katika seti ya kwanza na alikuwa katika hatarilakini alitoka nyuma kwa 3-0 katika seti ya pili.

Victoria mwenye umri wa miaka 31 katika fainali yake ya kwanza kubwa tangu 2013, alikuwa mbele kwa 5-3 kabla ya Naomi kushinda.

Naomi alipiga kelele za furaha akichukua alama yake ya pili kisha akajilaza kwa utulivu uwanjani na kutazama angani wakati anafikiria mafanikio yake ya hivi karibuni.

Kiwango chake kiliongezeka kwani Azarenka hakuweza kudumisha kiwango alichoonesha katika seti ya ufunguzi.

Mpambano huo ulihakikisha Naomi, ambaye alishinda 2018 US Open na 2019 Australia Open, anaendeleza rekodi yake ya kushinda kila fainali ya Grand Slam ambayo alicheza.

“Sitaki kukuchezesha katika fainali nyingine yoyote, sikufurahia sana hiyo, ilikuwa mechi ngumu sana kwangu,” Naomi alimwambia Azarenka kwa utani. Aliongeza: “Ilikuwa ya kunivutia kwa sababu nilikuwa nikikutazama ukicheza hapa nilipokuwa mdogo. Nilijifunza mengi, kwa hivyo asante,

Chanzo: HabariLeo