0

Namungo, Biashara zaanza na ushindi

Namungo, Biashara zaanza na ushindi

Mon, 7 Sep 2020 Source: HabariLeo

TIMU za Namungo FC ya Lindi na Biashara United ya Musoma zimeuanza vema msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/2021, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Gwambina FC ya Mwanza.

Katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, mkoani Lindi, bao pekee la Bigirimana Blaise alilofunga katika dakika ya 64 lilitosha kabisa kuwatoa kimasomaso Namungo FC kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo.

Kwenye Uwanja wa Karume, Musoma, Mara, bao lililofungwa na Kelvin Friday katika dakika ya 88 lilitosha kuwapa ushindi wa bao 1-0 Biashara United.

Mtibwa Sugar walitoka suluhu dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Gairo, mkoani Morogoro.

Raundi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bar itakamilishwa leo, wakati KMC itakuwa mwenyeji wa Mbeya City katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na Azam FC kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: HabariLeo