0

Nadal aangukia pua Paris Masters

Nadal aangukia pua Paris Masters

Mon, 9 Nov 2020 Source: HabariLeo

MCHEZA tenisi namba mbili duniani, Rafael Nadal ameangukia pua kwenye michuano ya Paris Masters baada ya Mjerumani, Alexander Zverev kumchapa kwa 6-4 7-5 kwenye nusu fainali mapema jana.

Ni ushindi wa pili mfululizo dhidi ya mshindi mara 20 wa Grand Slam kwa mchezaji huyo namba saba duniani Zverev, ambaye alipoteza mechi tano za mwanzo walizokutana.

Zverev, mshindi wa 13 wa michuano ya ATP aliimaliza mechi hiyo kwa saa moja na dakika 39.

Zverev aliyeshinda maraji mawili mwezi uliopita, jana usiku alitarajiwa kucheza fainali na Daniil Medvedev.

Mrusi huyo namba tatu Medvedev alimfunga mchezaji namba 10 Milos Raonic wa Canada kwa 6-4 7-6 (7-4) ndani ya saa moja na dakika 37.

Alimzidi kwa seti moja wakati wa mapumziko Nadal mwenye umri wa miaka 34 hakuwa tayari kulingana 3-3 katika seti ya pili na Zverev kwa haraka akamshangaza kwa kuwa mbele kwa 5-2.

Lakini mhispania huyo anaetumia mkono wa kushoto hakuwa tayari kushinda michuano hiyo ya Paris, akipoteza kwa David Nalbandian fainali ya mwaka 2007, akishinda michezo mitatu mfululizo.

Chanzo: HabariLeo