0

Mwakinyo atetea mkanda WBF kwa TKO

Mwakinyo atetea mkanda WBF kwa TKO

Sat, 14 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Mwandishi wetuDar es Salaam. Bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa mabara wa uzito wa Super Welter wa WBF baada ya kumchapa kwa TKO Jose Carlos Paz wa Argentina katika raundi ya nne.

Tofauti na mapambano mengine, Mwakinyo alianza pambano kwa kasi ya hali ya juu huku akimsukumia makonde makali mpinzani wake ambaye raundi ya kwanza alicheza kwa kujilinda zaidi huku akijibu mapigo

Raundi ya pili ilikuwa ngumu kwa Paz baada ya Mwakinyo kuamua kucheza zaidi na ngumi za tumbo huku akitumia ‘jab’ kwa staili ya ‘kudokoa’ na kujipatia pointi nyingi katika pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sport chini ya Mkurugenzi Kelvin Twissa.

Ngumi hizo zilimchanganya sana Muargentina huyo na kuamua kucheza kwa kuvamia ambapo ilimlazimu Mwakinyo kuanza kurudi nyuma ili kumkwepa.

Mtanzania huyo angeweza kupata ushindi wa KO katika raundi ya pili baada ya kumsukumia makonde kadhaa na Muargentina kuchanganyikiwa, lakini Mwakinyo hakuweza kutumia nafasi hiyo na kumpa nafasi Paz kuendelea na pambano,

Mwakinyo aliteleza na kuanguka chini katika raundi ya pili dakika ya pili na sekunde 33, hata hivyo aliweza kuendelea na pambano bila ya kuhesabiwa.

Chanzo: Mwanaspoti