0

Mshery: Kinda anayeifanya Mtibwa Sugar kuwa tofauti

Mshery: Kinda anayeifanya Mtibwa Sugar kuwa tofauti

Mon, 9 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

Nyuma ya kiwango cha kipa chipukizi wa Mtibwa Sugar, Aboutwalib Mshery (21) kuna mazito aliyoyapitia, yanafunza na kutoa machozi, akikumbuka tu hata kama alikuwa anajihisi uvivu kufanya kazi yake, anapata nguvu ghafla.

Upole wa sura yake, ingawa ukizungumza naye ni mtu anayependa ucheshi, pia ni kijana mwenye nidhamu na anapenda kusikiliza kwa umakini.

Mshery ameanza kikosi cha kwanza katika mechi nane kati ya tisa ambazo timu hiyo imecheza mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara huku akiruhusu mabao matano.

Kipa huyo ameonyesha kiwango kikubwa langoni hata kuwaweka benchi makipa wazoefu kama Shaban Kado na Said Mohammed ‘Nduda’ huku akijizolea mashabiki wengi wa soka ambao wamekuwa wakivutiwa na ubora wake langoni huku wengi wakimtabiria makubwa siku zijazo.

Baada ya kuichezea kwa mafanikio timu ya vijana ya Mtibwa Sugar hadi 2018 kocha aliyetimka katika kikosi hicho Zubery Katwila alivutiwa na uwezo wake na kumpandisha katika kikosi cha wakubwa msimu uliopita na mechi yake ya kwanza kuanza golini ilikuwa ya Februari 15, lakini bahati mbaya akaumia ndani ya dakika chache baada ya mpira kuanza.

Anamuogopa zaidi Bocco

Chanzo: Mwanaspoti