0

Mgombea Ubunge ataka vijana wanufaike na ajira michezoni

Mgombea Ubunge ataka vijana wanufaike na ajira michezoni

Mon, 14 Sep 2020 Source: HabariLeo

MGOMBEA wa Ubunge wa kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Profesa Kitila Mkumbo amewaasa wanamichezo kujituma kikamilifu ili kujiletea matokeo chanya katika sekta hiyo.

Profesa Mkumbo ameyasema hayo aliposhiriki kutazama mchezo wa mpira wa miguu (Ndondo Cup) kati ya Zofa Fc na Mabibo Market ambayo ilishinda magoli 2-1 dhidi ya Zofa.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Urafiki(Kinesi), Profesa Mkumbo alisema michezo ni ajira hivyo ni vyema wanamichezo wote wakajituma wakati wote wanapopata nafasi.

Alisema michezo imekuwa sehemu kuu ya ajira kwa wanaozingatia na kujituma na kusisitiza kuwa njia pekee kwa vijana ni kuhakikisha wanashiriki ipasavyo.

Katika mchezo huo Profesa Mkumbo alipewa heshima ya kukagua timu zote mbili na kuzungumza na wachezaji hao kabla ya kuanza kwa mchezo huo ulipushuhudiwa na wamia ya mashabiki.

Chanzo: HabariLeo