0

Mauya ampa tano Wawa

Mauya ampa tano Wawa

Wed, 11 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIPA ASSAKIUNGO wa Yanga, Zawadi Mauya amemtaja beki wa Simba, Pascal Wawa kwamba  anacheza soka  kwa kutumia akili ya kusoma washambuliaji  wa upinzani kabla hawajafika eneo la kipa wao, jambo analokiri aliliona kwenye mechi ya watani wa jadi.

 

Mauya ameliambia Mwanaspoti Online jana Jumanne Novemba 10, 2020 kwamba Wawa ni kati ya wachezaji wa Simba  waliofanya majukumu makubwa kwenye mechi ya watani wa jadi, iliopigwa Novemba 7.

 

Amesema alimuona Wawa jinsi ambavyo alikuwa anaokoa hatari za washambuliaji wa Yanga kwa kutumia akili na nguvu, jambo analoona ana kitu chakuisaidia Simba kwenye ligi ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Chanzo: Mwanaspoti