0

Makomandoo Simba wazuia mashabiki

Makomandoo Simba wazuia mashabiki

Fri, 6 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

KIKOSI cha Simba kinaendelea na mazoezi jioni ya leo Ijumaa kujiandaa na mechi dhidi ya watani zao Yanga ambayo itachezwa kesho Jumamosi katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Katika mazoezi hayo ya Simba yaliyofanyika Uwanja wa Mo Bunju Arena kulikuwa na makomandoo waliovaa vitambulisho vya timu hiyo.

Makomandoo hao ambao walikuwa wawili wakizunguka maeneo yote waliyokuwa wamesimama mashabiki kufuatilia mazoezi hayo.

Wakiwa wanafuatilia mashabiki hao makomandoo walikuwa wanawaambia si ruhusa kwa shabiki yeyote kupiga picha wala kuchukua video kwa chochote ambacho kilikuwa kinaendelea uwanjani.

Makomandoo hao hawakuishia hapo waliwataka mashabiki wote waliojitokeza kukaa katika uzio wa pili na si ule wa kwanza ambao ni karibu na eneo la uwanja.

Mara zote ambazo Mwanaspoti Online hutembelea mazoezi hayo ya Simba mashabiki husimama na kukaa katika uzio wa kwanza ila safari hii hawakuruhusiwa.

Chanzo: Mwanaspoti