0

Makocha matumbo joto robo fainali RBA

Makocha matumbo joto robo fainali RBA

Thu, 17 Sep 2020 Source: Mwanaspoti

By Imani MakongoroDar es Salaam. Mambo yameanza kunoga Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), ambayo imefikia hatua ya robo fainali kwa vigogo, JKT, Ukonga Kings, ABC, Vijana, Pazi, Oilers, Kurasini Heat na Savio kufuzu.

Mechi za kwanza za robo fainali zitachezwa Septemba 23 kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini.

Pazi itachuana na Oilers, Ukonga Kings itaonyeshana uwezo na JKT, Vijana dhidi ya ABC na Savio itachuana na Kurasini Heat, timu itakayoshinda mechi mbili mfululizo itakata tiketi ya nusu fainali, la sivyo, mshindi wa mechi ya tatu ‘game three’ ndiye atafuzu. Utaratibu huo utatumika pia kwenye mechi za nusu fainali na fainali.

JKT ndiyo timu pekee ambayo ilicheza mechi zote 15 bila kufungwa na kuongoza msimamo ikiwa na pointi 30, ikifuatiwa na ABC, ambayo ilishinda mechi 12 na kufungwa mechi tatu.

Makocha na wachezaji nyota wa timu hizo wameanza kupiga hesabu ya kufuzu kucheza nusu fainali.

Mody Mbwana, kocha wa Pazi alisema licha ya uzoefu wao kwenye historia ya kikapu, watacheza mechi hiyo kwa malengo.

Chanzo: Mwanaspoti