0

MSAIDIZI KATIBU MKUU WA OLYMPIC ANAZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI

MSAIDIZI KATIBU MKUU WA OLYMPIC ANAZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI

Wed, 4 Nov 2020 Source: Zanzibar 24

Msaidizi katibu mkuu wa kamati ya Olympic Tanzania Suleiman Mahmoud Jabir akizungumza na Waandishi wa habari za Michezo kwa upande wa Zanzibar, Leo Novemba 4,2020 amesema kamati ya Olimpiki Tanzania inategemea kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa kuingoza kamati hiyo kwa miaka minne.

Uchaguzi huo utafanyika Jijini Dodoma Disemba 12/2020 (TOC) imesema Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaomaliza muda wao wa Uongozi hawatopiga kura kama inavyoeleza (Ibara 16.0.8).

Fomu za Uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea zitaanza kuchukuliwa katika ofisi za TOC za Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia 6/11/2020 na kurejeshwa 20/11/2020 na kwa nafasi ya Urais , Makamo wa Rais, Katibu Mkuu Msaidizi, Mhazini Mkuu, na Mhazini Mkuu msaidizi watalipia ada ya shilingi laki mbili na hamsini kwa upande wa nafasi za wajumbe wao watalipia ada ya shilingi laki mbili.

TOC imewachaguwa wajumbe watatu kwaajili ya kusimamia uchaguzi ni

Lloyd Nchunga – Tanzania Bara

Harrison Chaulo – Tanzania Bara

Abdallah Juma Mohammed – Zanzibar

Kwa upande wa Zanzibar fomu zitarejeshwa uwanja wa Amani Zanzibar Kabla ya saa 10:00 jioni Alasiri.

STORY NA HAMID KHAMIS:ZANZIBAR24.

Chanzo: Zanzibar 24