0

MO’: HATUNA MPANGO NA MUKOKO

F1c26d77da955509d6e8155b7b4a605d MO’: HATUNA MPANGO NA MUKOKO

Tue, 17 Nov 2020 Source: HabariLeo

WAKATI Simba ikisisitiza kumalizana na mchezaji wake Cletus Chama, klabu hiyo imesema haina mpango wa kumsajili mchezaji wa wapinzani wao Yanga, Tonombe Mukoko.

Kwa mujibu wa klabu hiyo, Chama ameingia mkataba wa miaka miwili mpaka mwaka 2023.

Aidha, klabu hiyo imesema haina mpango wa kumsajili Mukoko na inashangaa tetesi za Simba kumtaka mchezaji huyo zinatoka wapi kwani hawana hata nia ya kumsajili mchezaji huyo kutoka Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ alisema wameshamalizana na Chama na wanashangaa klabu nyingine kumuweka kwenye majarida wakimvalisha jezi zao, jambo ambalo linawapa ruhusa ya kuwashtaki wakitaka.

Juzi aliyekuwa msemaji wa Yanga Dismas Ten aliweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram tangazo la Jarida la Yanga linalomuonyesha Chama akiwa wamevalia jezi za Yanga.

Suala hilo lilizua taharuki kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wanajua mchango kiungo huyo raia wa Zambia anaoutoa kwenye kikosi hicho.

“Chama hajaenda popote tumesaini naye mkataba wa miaka miwili tena tumemalizana naye mali ya Simba ana mapenzi mazuri na Simba na kwenye ligi amechukua tuzo zaidi ya tano, anafahamu falsafa ya timu ndio sababu tumemuongezea mkataba,” alisema.

Dewj alisema taarifa za Chama kuingia mkataba na watani zao ni za kupuuzwa kwani hazina ukweli wowote.

Pia alisema kuanzia wiki ijayo kupitia kwenye mitandano yao ya kijamii wataanza kurusha taarifa rasmi za wachezaji wao waliwaongezea mkataba na wale walipendekezwa kuachwa na kocha.

Chanzo: HabariLeo