0

Kwa Yanga hii

Mon, 7 Sep 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

RAHA ya mpira chenga bwana, hivyo ndivyo ilivyofanya timu ya Wananchi Yanga katika mchezo wake wa kwanza wa msimu mpya wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo ulianza saa 1:00 usiku, ambapo Yanga ilianza kwa kucheza mpira wa vyenga hali ilyosababisha mashabiki kulipukwa kwa furaha.

Mchezaji wa Yanga Feisal Salum ndio alionekana kukonga nyoyo za mashabiki kwa jinsi alivyokuwa anauchezea mpira.

Prisons ilionekana kuwa nyuma ikijaribu kuisoma Yanga na dakika ya nane Yanga ilipoteza mpira eneo la kati kati baada ya uzembe kiungo wake wa kati Zawadi Mauya.

Mpira huo ulinaswa na beki wa kulia wa Prisons Michael Ismail ambaye alipiga krosi iliyomkuta mlinzi wa kati wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye pia alikosea na kuchoma kwa Lambart Sabiyanka aliyetumia ustadi kubwa kupita shuti ambalo lilimshindwa mlinda mlango wa Yanga na akaiandikia Yanga bao la kwanza.

Baada ya kufungwa Yanga ilionekana kutulia na kujipanga upya na kuanza kulisakama lango lango la Prisons.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz