0

Kaduguda awatupia dongo watani

Kaduguda awatupia dongo watani

Thu, 5 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIVER ALBERTMWENYEKITI wa Simba, Mwina Kaduguda sijui anawatafuta nini Yanga, amewaambia kuwa wamekuwa wakibahatisha tu kupata ushindi katika mechi zao kwani timu bora haiwezi kufunga bao moja moja tena la jioni muda ambao kuku wanakwenda kulala.

Akizungumza na Mwanaspoti Online jana umatano Novemba 4, 2020, Kaduguda alisema haihofii hata kidogo mechi ya keshokutwa Jumamosi kwani anaamini timu yake inakwenda kupata ushindi wa kishindo na timu pekee ambayo huwa anaihofia kwenye ligi ni Azam .

"Yanga ni watani zetu wa jadi lakini siwahofii kwani hawatuwezi. Azam ndio huwa naiogopa kwani imesajili vizuri na wanacheza mpira mzuri wa kuelewana.

"Kiufundi Yanga sio wazuri ila ni timu nzuri ya kawaida, kwani timu bora haiwezi kushinda bao moja moja katika mechi zake ina maana wanabahatisha.Tena ukitaka kujua wanabahatisha wanafunga mabao yao jioni muda ambao kuku wanakwenda kulala, sasa utailinganishaje timu hiyo na Simba ambayo inashinda mabao mengi katika mechi zake tena muda wowote'', alisema Kaduguda.

Kaduguda amekanusha habari za kuwa kuna msuguano ndani ya klabu hiyo kwa kusema mambo yako shwari na wanakwenda kuichapa Yanga wakiwa na umoja.

"Hayo maneno maneno ambayo watu wanachonga kuwa ndani ya klabu kuna mvurugano  si ya kweli kwani ni watu tu wameamua kuzusha wasiyoyajua

Chanzo: Mwanaspoti