0

KMC yaikaribisha Mbeya City

KMC yaikaribisha Mbeya City

Mon, 7 Sep 2020 Source: HabariLeo

UONGOZI wa KMC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Habibu Kondo kimefanya maandalizi yake ya mwisho jana kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa ni wa kwanza kwa timu hizi ndani ya msimu wa 2020/21.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala imeeleza kuwa maandalizi ya kikosi yamekamilika kwa asilimia 100.

"Hadi Sasa kikosi kimefanya maandalizi kwa asilimia 100 kipo tayari kwa ajili ya ushindani na kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City.

"Wachezaji wamejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho na mpaka sasa hakuna majeruhi ambaye yupo ndani ya timu hivyo imani ni kubwa kwa kikosi chetu kuweza kusaka pointi tatu kwenue mchezo wetu wa kesho ambao ni muhimu kwetu," amesema.

Mechi nyingine leo, Azam atakutana na Polisi Tanzania Katika mchezo utakaofanyika Azam Complex Chamazi.

Chanzo: HabariLeo