0

Jezi mpya United yazua gumzo

Wed, 9 Sep 2020 Source: habarileo.co.tz

KLABU ya Manchester United imezitambulisha jezi zao mpya zitakazotumika msimu wa 2020/21.

Hata hivyo, jezi hizo zenye muonekano wa pundamilia zimepokelewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wa mashetani hao wekundu wa England.

Licha ya baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United kutumika katika kutangaza jezi hizo akiwemo, Bruno Fernandez, Marcus Rashford na Scott McTominay, pia aliyekuwa mchezaji nyota wa klabu hiyo na mfanyabiashara, David Beckham ameonekana kuvaa jezi hiyo.

Mashabiki wanadai hazina muonekano mzuri wengine wakisema “Hata Beckham zimemfanya kutoonekana mzuri,” aliandika shabiki Mcasemarcus.

Prateek yeye lieandika: “Msajilini Sancho na sisi tutawasamehe kuhusiana na hiyo jezi yenu ya tatu.” Luis Parker aliandika: “Watu wataitumia jezi hii kukatiza barabarani.”

Shabiki mwingine, Reddevil76 alisema: “Kamwe sitaandika jina langu katika jezi hii ya kudhalilisha hata kama nitaipata bure.” Hayo ni maoni machache kati ya mengi yaliyotolewa na mashabiki wa United kuhusiana na jezi hiyo ya tatu iliyotambulishwa na klabu hiyo

Chanzo: habarileo.co.tz