0

Jeshi jipya Ligi Kuu Bara ndo hili hapa

Jeshi jipya Ligi Kuu Bara ndo hili hapa

Thu, 3 Sep 2020 Source: Mwanaspoti

By YOHANA CHALLETAYARI dirisha la usajili la wachezaji lilifungwa tangu Jumanne na sasa kilichobaki ni kuona namna nyota hao watakayoyafanya kwenye ligi itakayoanza wikiendi hii.

Ndani ya Ligi Kuu pekee tumeshuhudia wachezaji wakigeni 50 wakisajiliwa huku Azam na Simba zikisajili nyota 10, Yanga ikiwa na yota nane, Namungo FC saba, Biashara sita, KMC watatu, Kagera Sugar wawili wakati Dodoma, Mtibwa Sugar, Gwambina na Mbeya City wakiwa na nyota mmoja.

Katika usajili mengi yametokea hasa sakata la Benard Morisson aliyekuwa akiitumikia Yanga msimu uliopita lakini katika orodha ya usajili inaonekana yupo ndani ya Simba.

Mwanaspoti kama kawaida linakudondoshea kwa karibu nyota waliotua ndani ya vikosi vyote 18 vya Ligi Kuu ambavyo vinaanza kulisaka kombe la msimu huu Jumapili.

AZAM FC Alain Akono

Chanzo: Mwanaspoti