0

Ishu za Mwamnyeto zafichuka

Ishu za Mwamnyeto zafichuka

Tue, 3 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIPA ASSAKUMBE nidhamu anayoionyesha beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha msaidizi wa Lamine Moro, inatokana na baba yake mzazi aliyefichua siri uwa imeanzia kwenye misingi aliyoijenga ndani ya familia yake.

Baba mzazi wa beki huyo, Mwamnyeto Nondo alisema kuna misingi ambayo aliijenga katika familia yake ambayo kijana wake hatakiwi kuivunja hata kama yupo nje ya familia hiyo.

Alisema aliwafundisha namna nidhamu unavyoweza kumpa hatua ya maendeleo na akaonekana bora katikati ya wengine, jambo alilosema linaenda sawa mpaka sasa kwani, anafuatilia kila anachokifanya uwanjani.

“Nilianza kuwafundisha nidhamu tangu wakiwa wadogo kwa kila kitu walichokuwa wanakifanya hapa nyumbani kabla ya kuvuka mipaka ya familia nyingine, naamini Yanga wasingekurupuka kumpa beji hiyo angekuwa hajielewi,” alisema na aliongeza kuwa,

“Niliposikia kapewa unahodha nilifarijika sana, nikampigia simu kumwambia uongozi unahitaji busara ili kutatua mambo na kuwafanya wenzake wakiwa wamoja na sio kujiona yeye ndiye yeye,” alisema.

WANAFURAHIA MAISHA

Chanzo: Mwanaspoti