0

Hiki ndicho alichokiona Adam Adam Taifa Stars

Hiki ndicho alichokiona Adam Adam Taifa Stars

Mon, 9 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By OLIPA ASSASTRAIKA wa JKT Tanzania, Adam Adam amesema kujumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kinachojiandaa  kucheza  mechi  ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Tunisia, Novemba 13 kimemuongezea kujiamini zaidi.

Kocha wa Taifa Stars, Ndayiragije Etienne amemuita mchezaji huyo kwenye kikosi chake akiwa na mabao 6 kwenye msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo ni mzawa anayeongoza sawa na mchezaji wa kigeni wa Azam FC, Prince Dube.

Adam ameliambia Mwanaspoti Online, leo Jumatatu Novemba 9, 2020 kwamba ni faraja kwake kuona anachokifanya kinaonekana na kocha wa Stars, kitu kinachomjengea ari yakujituma zaidi na kuamini kutimiza ndoto zake.

"Wapo wachezaji wengi wa nafasi ninayocheza, ambao wangeweza kuitwa hivyo kujumuishwa mimi kwenye kikosi hicho, nimejisikia faraja na imenipa nguvu ya kuendelea kupambana zaidi," amesema Adam Adam na ameongeza kuwa;

"Hakuna mchezaji ambaye hapendi kuchezea timu ya taifa lake, ndio maana kwangu naifurahia nafasi hii na natamani siku moja itokee nije kuwa tegemeo kwenye kikosi hicho,"amesema.

Ukiachana na jinsi ambavyo amefurahia kuwa miongoni mwa wale ambao wanaunda timu hiyo, pia amesema atatumia fursa hiyo kujifunza mengi kwa wachezaji wenye mafanikio makubwa.

Chanzo: Mwanaspoti