0

Gwambina kuchanga karata nyumbani

Thu, 10 Sep 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

BAADA ya kivumbi cha mzunguko wa kwanza kwenye ufunguzi wa Ligi Kuu Bara, kuchezwa mwisho wa wiki iliyopita kesho Ijumaa ligi hiyo  itaendelea tena katika viwanja viwili tofauti.

Mechi ya kwanza  itazikutanisha Gwambina ambao watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Kagera Sugar wakati Azam itaikabili  Coastal Union kwenye Uwanja wa Chamazi Complex kuanzia saa 1:00.

Gwambina waliopanda daraja msimu huu wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0, dhidi ya Biashara United katika mchezo wa kwanza wakati wapiznani wao Kagera Sugar nao walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania.

Katibu wa Gwambina, Daniel Kilai amesema kutokana na ripoti ambayo ameipata kutoka katika benchi la ufundi uwanja waliotumia katika mechi na Biashara umewasababishia majeruhi ya wachezaji watatu.

“Kama uongozi maandalizi yapo vizuri na bahati nzuri Kagera ni timu ambayo tunaimudu kwani tumecheza nao mechi tatu za kirafiki tukiwa Ligi Daraja La Kwanza tuliwafunga mbili na kutoka nao sare mbili,” anasema Kilai.

Mechi  nyingine kesho  itakayonza saa 1:00 usiku itazikutanisha   Azam FC  dhidi ya  Coastal Union.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz