0

Familia ya bondia aliyepasuliwa fuvu yasimulia mazito

Familia ya bondia aliyepasuliwa fuvu yasimulia mazito

Thu, 17 Sep 2020 Source: Mwanaspoti

By IMANI MAKONGOROJUZI bondia Karim Ramadhani alipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huko Mikese mkoani Morogoro baada ya kuanguka na kuzimia akiwa mazoezini.

Bondia huyo alifariki akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Mloganzila, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kocha wa Gym ambayo bondia huyo alidondoka, Amosi Nkondo ‘Amoma’ amesema.

“Alikuja mazoezini, nilipomwambia kufanya mazoezi akasema kocha sijisikii vizuri, akaomba aruke kamba na kupiga begi ‘punching bag’ tu,” anasimulia kocha Amoma.

Anasema baada ya muda alidai kusikia kizunguzungu, lakini ghafla alidondoka na kupoteza fahamu.

“Tulimpa huduma ya kwanza pale na kumpeleka Palestina ambapo walishauri akafanyiwe kipimo cha kichwa na kutupa rufaa ya kwenda Mloganzila,” anasimulia kocha Amoma kwa huzuni.

Chanzo: Mwanaspoti