0

Dakika 90 zaigawa Simba, Yanga

Dakika 90 zaigawa Simba, Yanga

Fri, 6 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By THOBIAS SEBASTIANKUELEKEA mechi ya kesho Jumamosi kati ya Yanga na Simba ambayo kwenye Ligi Kuu ndiyo mechi inayoongoza kuwa msisimko mkubwa kwa mashabiki kutokana na ushindani wa timu hizo ambapo kocha Adolf Rishard ametoa neno.

Rishard anasema Simba ni wataalamu wa kufunga mabao mengi kipindi cha kwanza na wamekuwa wakifanya hivyo ili kutawala mchezo jambo ambalo wanafanikiwa wakati Yanga wao mabao yao mengi hufungwa kipindi cha pili.

"Dakika 15 za mwanzo, katikati au mwisho wa mechi timu ikifanya vizuri naipa nafasi kubwa ya kuondoka na pointi tatu kwani ndio watakuwa wameutawala mpira na kufanya mambo mengi ya kiufundi ambayo yatakuwa yanakubali upande wao," anasema Rishard ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo miaka ya nyuma.

Kiungo wa zamani wa Simba, Mlage Kabange anasema siku zote zinapokutana timu hizo mbili rekodi zinaweza kuwekwa pembeni kwani timu inayooneka kuwa bora kwa matokeo ya mechi zilizopita na wachezaji wao walivyo lakini wakapoteza pambano hilo.

"Yanga wamefanya mabadiliko ya Benchi la Ufundi na hata kikosi chao kimekuwa na ingia toka jambo ambalo linachingia wao kukosa muunganiko na hata mabao wanayofunga mengi ni ya kipindi cha pili ingawa katika mechi kubwa za namna hii lolote linaweza kutokea," amesema Kabange.

Kiungo wa zamani wa Yanga, Salum Telela anasema timu zote mbili zipo vizuri eneo la kiungo lakini Yanga ni bora eneo la kushambulia tofauti na Simba ambao wameonekana kuwa na washambuliji wenye uwezo wa kufunga.

Chanzo: Mwanaspoti