0

Bondia Itaba agomea matokeo ya kupigwa, TPBRC yabadili na kuweka

Bondia Itaba agomea matokeo ya kupigwa, TPBRC yabadili na kuweka

Sat, 14 Nov 2020 Source: Mwanaspoti

By Mwandishi wetuDar es Salaam. Bondia Hussein Itaba jana usiku aligoma kutoka ulingoni akigomea matokeo dhidi ya mpinzani wake kutoka DR Congo Alex Kabangu ambapo awali alitangazwa kuwa amepoteza kwa pointi.

Katika pambano hilo, Jaji Ali "Champion" Bakari na Ibrahim Kamwe walitoa sare ya pointi 94-94 kila mmoja huku refa na jaji mkongwe nchini John Chagu alitoa ushindi kwa Kabangu kwa pointi 94-95.

Matokeo hayo yalipingwa na Itaba kuwa jaji mmoja hawezi kutoa maamuzi ya pambano lao la uzito wa Super Middle na kusababisha malumbano na bondia aligomea kutoka ulingoni.

Hoja ya Itaba iliungwa mkono na gwiji la ngumi za kulipwa nchini, Emmanuel Mlundwa na kaimu rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) Aga Peter kupanda ulingoni na kubadili matokeo hayo katika pambano ambalo lilikuwa na upinzani mkubwa huku kila bondia akianguka mara moja katika raundi tofauti.

Peter alisema kuwa matokeo hayo yakitumwa boxrec, TPBRC itaingia katika matatizo mengine kwani ni kinyume na sheria na kuchochea hali iliyoposasa ambapo wanahangaikia mtandao huo wa kuweka rekodi za mabondia kurejesha rekodi za mabondia wa Tanzania.

Wakati matokeo hayo yanatangazwa, bondia Kabangu hakuwepo ulingoni na mara baada ya kupata taarifa hizo,alishangazwa sana.

Chanzo: Mwanaspoti