0

Barbara: Simba subirini vitendo

Wed, 16 Sep 2020 Source: mwanaspoti.co.tz

By Majuto Omary Dar es Salaam. Ofisa mtendaji mkuu mpya wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa yeye ni mtu wa kufanya kazi kwa vitendo na wala si maneno.

Barabara alisema hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika wiki iliyopita.

Alisema kuwa yeye ni mtu mkali na anayejali muda katika kufanya kazi zake kwa wakati.

“Mimi ni mtu wa kufanya kazi kwa vitendo na wala sio kwa manenomaneno, nataka ufanisi zaidi na mpaka sasa najivunia kuwa mtu wa hivyo,” alisema Barbara.

“Niliwaambia wazazi wangu kuwa nataka kufanya kazi za kuitumikia jamii, nimepitia taasisi kadhaa mpaka kuwa mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, kote huko nimekuwa mtu wa vitendo.”

Alisema kuwa akiwa anafanya kazi katika Taasisi ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation), alikuwa na cheo cha mkuu wa wafanyakazi - kazi ambayo ilimfanya mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kumteua kuwa mmoja wa wakurugenzi wa klabu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz