0
Menu
Infos

Wanafunzi 10 waliofanya vizuri darasa la saba

3ff935ea32c54f19534e6dc9da185708 Wanafunzi 10 waliofanya vizuri darasa la saba

Sat, 21 Nov 2020 Source: HabariLeo

Baraza la Mitihani la Taifa nchini (Necta), limemtaja mwanafunzi Herrieth Japhet Josephat aliyehitimu shule ya msingi Graiyaki iliyopo Mara, kuwa ndiye kinara katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi.

Herrieth anakuwa msichana pekee kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, waliotajwa na baraza leo Jumamosi, Novemba 21, 2020 wakati Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde akitoa taarifa ya matokeo hayo.

Angalia hapa matokeo ya Darasa la Saba

Alimtaja aliyeshika nafasi ya pili kuwa ni Huma Masala Huma kutoka shule ya msingi Kwema Morden ya Shinyanga na nafasi ya tatu ikienda kwa Gregory Mtete Alphonce kutoka Twibhoki shule ya msingi iliyopo mkoani Mara. Aliyeshika nafasi ya nne ni Nyambina Musa Nyambina kutoka shule ya msingi Graiyaki iliyopo Mara pia.

Andrew Elias Mabula kutoka shule ya msingi Kwema Morden ya Shinganya, ameshika nafasi ya tano, Jonas Nyamataga Ayubu (Little Flower) Mara, Emmanuel Kashinje Paul (Kwema Morden) Shinyanga, Emmanuel Peter Marwa (Kwema Morden) Shinyanga, Prosper Aspenas Tumbo (God’s Bridge) Mbeya na nafasi ya 10 ilikwenda kwa Yesaya Mnkondo Bendera kutoka shule ya msingi God’s Bridge ya jijini Mbeya.

Baraza hilo limetangaza kuzifutia matokeo Shule 38 kutokana na udanganyifu. Shule hizo 38 kati ya 17,329 ambazo zilifanya mtihani, ziligundulika kukiuka Kanuni na Usimamizi wa Mitihani baada ya Wanafunzi 1,059 kuwa na ufanano wa majibu. Shule hizo ni kutoka mikoa ya Geita, Morogoro, Simiyu, Arusha na Tabora.

Chanzo: HabariLeo