0
Menu
Infos

Wakulima watakiwa kuzingatia kanuni kilimo bora

Wakulima watakiwa kuzingatia kanuni kilimo bora

Sat, 21 Nov 2020 Source: HabariLeo

Wakulima wa Pamba wametakiwa kuzingatia kanuni 10 za kilimo bora cha zao hilo kwa kupata kilo 800 hadi 1200 kwa ekari.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Said Nkumba wakati akizindua rasmi msimu wa zao hilo kwa mwaka 2020/2021 kwa vitendo katika shamba darasa kwenye kata ya Bulega wilayani humo.

Amesema kwa kufuata kanuni hizo taifa litapata fedha nyingi za kigeni kwa kuuza Pamba iliyo bora nje ya nchi na kuinua pato la mkulima mmoja mmoja.

Katika hatua nyingine Nkumba amewataka viongozi wa vyama vya ushirika vinavyosimamia zao hilo (AMCOS) kuwa waadilifu ili wakulima wapate fedha inayoakisi kiasi cha jasho walilovuja.

Chanzo: HabariLeo