0
Menu
Infos

Wahamiaji haramu wahukumiwa jela 

7bc4e726e35e42464491b50e6fd42657.jpeg Wahamiaji haramu wahukumiwa jela

Fri, 20 Nov 2020 Source: HabariLeo

Wahamiaji haramu 36 kutoka nchini Ethiopia na Somalia wamehukumiwa kulipa faini ya Tsh. 600,000 kila mmoja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuingia nchini bila kibali.

Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu amesoma hukumu hiyo hii leo mara baada ya watuhumiwa hao kusomewa mashtaka mawili ya kuishi nchini bila kibali na kukubali kufanya makosa hayo.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Shaidi aliwapa washtakiwa hao nafasi ya kujitetea ili wapunguziwe adhabu hiyo ambapo wote kwa pamoja waliomba mahakama iwaonee huruma kwakuwa wameingia nchini kutoka na amani iliyopo baada ya kutoka nchi zenye vurugu.

Chanzo: HabariLeo