Serikali kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi vitendea kazi
Mon, 22 Feb 2021
Source: HabariLeo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kutoa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi kadri inavyowezekana ili kuwawezesha askari nchini kote kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Majaliwa amebainisha hayo jana akiwa mkoani Lindi katika Kituo cha Polisi cha Mtama alipokuwa anakabidhi magari mawili kwa ajili ya jeshi hilo mkoani humo ili yawasidie kufanya doria.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amesema magari hayo yatawezesha shughuli za doria kufanyika kwa uhakika kitu kitakachosaidia kupunguza uhalifu.
Magari yaliyokabidhiwa ni Toyota Land Cruiser Pickup yenye namba za usajili PT 2615 na Toyota Land Cruiser V6 lenye namba za usajili PT 4378.
Chanzo: HabariLeo