0
Menu
Infos

Nitashirikiana na wadau-Dk Mwinyi

5cb2e19624aafdd0707461a56688a32c Nitashirikiana na wadau-Dk Mwinyi

Fri, 20 Nov 2020 Source: HabariLeo

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema yupo tayari kushirikiana na wadau wa michezo visiwani humo kuhakikisha michezo inarudi kwenye kiwango kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Rais Mwinyi aliyasema hayo jana mjini Zanzibar alipotangaza Baraza lake la Mawaziri.

Alisema pamoja na kukutana na wadau hao, yupo tayari kuangalia mambo yote mazuri yaliyoachwa kuyaendeleza na kubuni mapya.

“Michezo nimeizungumza sana kwenye kampeni zangu, nipo tayari kama nilivyosema awali kukaa pamoja na wadau wa michezo tuangalie kila ambalo ni la kujenga katika masuala ya michezo tulifanye.

“Na kama kulikuwa na mifano mizuri huko nyuma ya uanzishaji wa mashindano maalumu na utaratibu wa kufanya michezo uwe bora nipo tayari,”alisema Mwinyi.

Alisema jukumu hilo atampatia waziri husika ili kwa pamoja na wadau kuangalia mambo yote muhimu ili kuboresha sekta ya michezo.

“Nitampatia majukumu waziri pamoja na wadau kuangalia yaliyoachwa kama yalikuwa mazuri tuyaendeleze na tubuni mapya kuhakikisha michezo inarudi kwenye kiwango tulichokuwa nacho nyuma,”alisema Mwinyi.

Chanzo: HabariLeo