0
Menu
Infos

Mwinyi ashtukiza sokoni, ambana RC "kilio cha wafanyabiashara wameandamana" (+video)

Video Archive
Thu, 19 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi kushirikiana na Uongozi wa Jiji la Zanzibar pamoja na wafanyabiashara, kutafuta eneo muafaka kwa ajili ya wafanyabiashara waliopo eneo la Kijangwani.

Dk. Mwinyi ametoa agizo hilo wakati alipofika eneo la kibiashara la Kijangwani, Wilaya Mjini Unguja na kuzungumza na wafanyabiashara wa hapo ambao wamekuwa katika utaratibu wa Serikali wa kuhama eneo hilo ili kupisha mradi wa kituo cha Usafiri.

Amewataka viongozi wa taasisi hizo kufanikisha agizo hilo mapema iwezekanavyo, sambamba na kuliwekea miundo mbinu muhimu inayohitajika ili kuwawezesha wafanyabaishara hao kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

TAZAMA MTITI WA NGUVU BOBI WINE AKIKAMATWA KISA KUJAZA WATU KWENYE KAMPENI

Chanzo: Millard Ayo