0
Menu
Infos

Mwinyi aibua mapya "Nimewaachia nafasi ACT Wazalendo za Mawaziri" (+video)

Video Archive
Thu, 19 Nov 2020 Source: Millard Ayo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi, ametangaza baraza jipya la Mawaziri katika Serikali yake huku akiacha kutangaza majina ya Mawaziri katika Wizara mbili na kusema kuwa ma Naibu Waziri atawachagua itakapobidi.

“Baada ya kukamilika kwa uchaguzi na ACT Wazalendo, kupata zaidi ya asilimia 10, tuliwaandikia barua ili walete jina la Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuwa jina bado halijafika lazima tuache wazi” Dkt. Mwinyi

“Nimeacha nafasi mbili za mawaziri wa chama cha ACT Wazalendo endapo watakuwa tayari lakini mpaka leo hawajaenda kusajiliwa na lazima tuwape muda wa kikatiba”, Dkt. Mwinyi

Chanzo: Millard Ayo