0
Menu
Infos

Makamu wa Rais afungua mkutano wa uwekezaji sekta ya madini

Da8b917ae19f390b68b7b1219f7be4ed Makamu wa Rais afungua mkutano wa uwekezaji sekta ya madini

Mon, 22 Feb 2021 Source: HabariLeo

Makamu wa Rais, Samia Suluhu leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania 2021 ambapo amewataka wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja kuwekeza katika sekta hiyo.

Akizungumza katika hotuba yake Jijini Dar es Salaam, Suluhu amebinisha kuwa kwa mwaka jana sekta hiyo ndiyo iliongoza kwa ukuaji kwa 17.7% pamoja na uuzaji wa vito vya thamani kubwa nje ya nchi hivyo kuvutia wawekezaji wengi.

“Niungane na wito wa kiongozi wetu Rais Magufuli kuwakaribisha nchini wale wote mnaofuatilia kongamano hili (kwa njia ya video) na wengine wenye nia ya kuja kuwekeza katika sekta hii hapa nchini inayokuwa kwa kasi kubwa sana “ amesema Suluhu.

Aidha, Suluhu amesema kuwa pamoja na janga la corona lililokumba dunia kuipa changamoto ya uzalishaji na soko la uhakika sekta hiyo lakini mwaka jana Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tano barani Afrika ambazo ni wazalishaji wakubwa wa madini ya dhahabu.

-

Chanzo: HabariLeo