0
Menu
Infos

Kamanda Sirro atoa ufafanuzi vurugu Mtwara

Kamanda Sirro atoa ufafanuzi vurugu Mtwara

Thu, 19 Nov 2020 Source: HabariLeo

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea mkoani Mtwara, zilizofanywa na kikundi cha Ahlu Sunnah Wal-Jamaah (ASWJ) kutoka nchini Msumbiji, umefikia hatua nzuri kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro amesema wamegundua kuwa kuna baadhi ya watanzania wanahusika na vurugu hizo. “Ukiona kama pale Kitaya walikuwa wanachoma nyumba moja nyingine wanaruka hii inaonyesha kulikuwa kuna mtu kutoka nchini kwetu aliyekuwa anawonyesha sehemu ya kuchoma” amesema Kamanda Sirro. Amesema Jeshi la Polisi linawashikilia baadhi ya watu ambao wamekiri kuhusika kukileta kikundi hicho na kuwasaidia kuwaonyesha maeneo ya kutekeleza uhalifu. Aidha, Kamandaa Sirro ametoa rai kwa wazazi na walezi hasa waishio maeneo ya mpakani kwenye mkoa huo kuwahasa watoto wao waache kutumika na kikundi hicho kwakuwa lengo lao sio zuri.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema uchunguzi kuhusu vurugu zilizotokea mkoani Mtwara, zilizofanywa na kikundi cha Ahlu Sunnah Wal-Jamaah (ASWJ) kutoka nchini Msumbiji, umefikia hatua nzuri kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, Kamanda Sirro amesema wamegundua kuwa kuna baadhi ya watanzania wanahusika na vurugu hizo. “Ukiona kama pale Kitaya walikuwa wanachoma nyumba moja nyingine wanaruka hii inaonyesha kulikuwa kuna mtu kutoka nchini kwetu aliyekuwa anawonyesha sehemu ya kuchoma” amesema Kamanda Sirro. Amesema Jeshi la Polisi linawashikilia baadhi ya watu ambao wamekiri kuhusika kukileta kikundi hicho na kuwasaidia kuwaonyesha maeneo ya kutekeleza uhalifu. Aidha, Kamandaa Sirro ametoa rai kwa wazazi na walezi hasa waishio maeneo ya mpakani kwenye mkoa huo kuwahasa watoto wao waache kutumika na kikundi hicho kwakuwa lengo lao sio zuri. “Kiujumla hali ya nchi yetu ni shwari hatuna matukio makubwa ya uvunjifu wa amani kuna changamoto kidogo katika matukio ya udhalilishaji ambayo yanaonekana kuongezeka hasa makosa ya kubaka na kulawiti” ameongeza IGP Sirro

Chanzo: HabariLeo