0
Menu
Infos

DK. HUSSEIN ATOA MIEZI MITATU KWA UONGOZI WA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

DK. HUSSEIN ATOA MIEZI MITATU KWA UONGOZI WA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

Thu, 19 Nov 2020 Source: Zanzibar 24

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussen Ali Mwinyi ametoa miezi 3 kwa Uongozi wa Hospitali ya rufaa Mnazi mmoja  kuhakikisha wanatoa huduma zinastahili kwa wagonjwa .

Dk. Hussein ametoa maagizo hayo leo Novemba 18,0202 mara baada ya kufanya ziara ya kushutukiza katika Hospital hiyo kufuatia kuwepo kwa lalamiko kutoka kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Aidha Dk.Hussein amesema hakuridhishwa hata kidogona utendaji kazi wao na huduma wanazopatowa haziendani na jina la hospitali hiyo .

Katika ziara yake hiyo Dk. Hussein ametembelea vitengo mbalimbali na kusikiliza changamoto za  wagonjwa ikiwemo  kitengo cha upasuaji ,sehemu ya kuhifadhia dawa kitengo cha mifupa pamoja na kutembelea jengo jipya la upasuaji ambalo bado halijaanza kazi .

Hata hivyo Dk. Husein amewataka wafanyakazi wa hospitali kuhakikisha wanavaa vitambulisho vyao vya kazi wakati wakiwa kazini ili kusaidia wagonjwa wawafahamu pia iwe rahisi kuwawajibisha wasiwajibika.

” Baabdhi ya watoa huduma wamekuwa na kauli chafu kwa wagonjwa hivyo inakuwa vigumu kuwaripoti taarifa zao kutokana na kutowatambua majina “ ” Nashangazwa na huduma mbovu zinatolewa na hospital hii kwani Wizara ya Fedha imetoa zaidi ya bilioni 3 kwa mwezi Ogasti na Septemba lakini bado hospital inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa dawa ,ukosefu wa vifaa vya matibabu ikiwemo vitanda  na mashuka ” Dk. Hussein.

Sambamba na hayo Dk. Hussein ameahidi kurudi na kuzungumza na Madaktari na wauguzi wa hospitalini hapo ili kujua kama haki zao wanapatiwa kama inavyotakiwa baada ya kugundua kasoro nyingi zilizomo katika hospitali hiyo .

Chanzo: Zanzibar 24