0
Menu
Infos

DK. HUSSEIN: ACT TULIWANDIKIA BARUA KWAMUJIBU WA SHERIA

DK. HUSSEIN: ACT TULIWANDIKIA BARUA KWAMUJIBU WA SHERIA

Thu, 19 Nov 2020 Source: Zanzibar 24

“Kuhusu kukutana na Maalim Seif kama Mtu mwenye nafasi ya kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Kwanza, tuliwaandikia kwa mujibu wa Katiba kama wako tayari tuendelee,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pia tuliwaandikia waapishwe, sisi tumetimiza wajibu wetu”-Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akitangaza Baraza la Mawaziri

“Niliahidi maridhiano, kwenye Kampeni nilisema tunataka Wazanzibar tuwe pamoja na kutekeleza Katiba, ACT walipata zaidi ya 10%, tukafuata matwaka ya Kikatiba kwamba watupe jina la Makamu wa Kwanza wa Rais, kwakuwa jina halijafika nafasi tumeiacha wazi”-MWINYI

“Kuhusu kutokuwa na Mpinzani katika Baraza la Mawaziri, upande wa Baraza la Mawaziri nimeacha baadhi ya nafasi wazi, Wabunge wa ACT hawajaenda kuapishwa, kwahiyo lazima tuwape muda wao Kikatiba, tumewaandikia pia kuwaomba wakaapishwe” -MWINYI

Chanzo: Zanzibar 24