0
Menu
Infos

Chuo Kikuu Mzumbe chafanikisha ujenzi wa ghofora

Chuo Kikuu Mzumbe chafanikisha ujenzi wa ghofora

Fri, 20 Nov 2020 Source: HabariLeo

Kupitia mapato ya ndani, Chuo kikuu Cha Mzumbe kilichopo mkoani Morogoro kimefanikiwa kujenga Jengo la kisasa la ghorofa tatu kwa gharama ya Sh bilioni 3.1 na ujenzi wake umakamilika kwa asilimia 100.

Makamu mkuu wa Chuo kikuu hicho, Profesa Lughano Kusiluka amesema hayo wakati akizungumzia mafanikio ya miaka mitano ya awamu ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano kuhusu uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya elimu.

Profesa Kusiluka ,amesema kuwa Jengo hilo lina madarasa manne yenye uwezo wa kila moja kukaa wanafunzi 100 ,kumbi mbili za mihadhara ambao kila mmoja una uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 na ofisi za wafanyakazi wa chuo wapatao 50.

Makamu mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe ,amesema jengo hilo limejengwa kutokana na kubana matumizi na makusanyo ya mapato ya ndani ya Chuo na kujengwa makandarasi wa Suma JKT,na kwa sasa kilichobaki ni kuwekwa samani.

Chanzo: HabariLeo