0
Menu
Infos

CCM yawacharukia wagombea wa Halmashauri

Fdf352c02ff38889ede650da2109d5fe CCM yawacharukia wagombea wa Halmashauri

Fri, 20 Nov 2020 Source: HabariLeo

Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitasita kufanya mabadiliko kwa wagombea wa nafasi za umeya na uenyekiti wa halmashauri za wilaya, miji na majiji watakaopata nafasi ya uongozi, baada ya mchakato wa kupiga kura, ikiwa watashindwa kuendana na kasi ya Rais Dk John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema kuwa katika kipindi cha awamu ya pili ya Serikali ya awamu ya tano, hakutakuwa na mzaha kwa kiongozi atayeshindwa kushughulikia utatuzi wa kero za wananchi.

“Mnafahamu tuna siku 1800 ipate kutimia miaka mitano hivyo hatuna muda wa kupoteza kwa kipindi hiki mnatakiwa kufanya kazi usiku na mchana kwenye kutatua kero za wananchi” amesema Polepole.

Amefafanua kuwa wagombea wa nafasi ya umeya waliojitokeza Jiji la Dar es salaam ni tisa, Arusha waliojitokeza ni 11, Dodoma saba, Tanga sita, Mwanza saba, na Mbeya ni 10.

Chanzo: HabariLeo